Washirika wa Magharibi waitaka Israeli kujiepusha na hatua zitakazozidisha mgogoro

 

Macho yote yanaelekezwa kwa Israel kuona jinsi inavyojibu mashambulio ya wikendi ya Iran ya droni na makombora lakini washirika wake wameitaka iepuke kuzidisha mzozo huo

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock anasema Israel "imeshinda kwa kujilinda" katika ugomvi wake na Iran, na lazima kusiwe na ongezeko la mzozo katika eneo hilo.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anaungana na wito wa kudumisha utulivu na kusema nchi yake itafanya kila linalowezekana kuepusha kuongezeka kwa mgogoro.

Na kama tulivyoripoti hapo awali,Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza David Cameron aliiambia BBC kwamba alifikiri Israel "ilikuwa na haki kabisa" kujibu Iran - lakini akahimiza nchi hiyo kuwa makini na "kufikiri kwa kichwa, siokwa moyo".

Urusi na China zataka kujizuia baada ya Iran kuishambulia Israel

Pamoja na washirika wa Israel, nchi zinazotajwa kuwa na mafungamano ya karibu zaidi na Iran zimezitaka pande zote mbili kujizuia.

Urusi ilijiepusha na kuikosoa hadharani Iran juu ya shambulio hilo, lakini ilishiriki wasiwasi juu ya hatari ya kuongezeka kwa mzozo.

"Kuongezeka zaidi hakutakidhi maslahi ya mtu yeyote," msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov alisema kuhusu vita katika Mashariki ya Kati.

Wizara ya mambo ya nje ya China pia ilitoa wito wa utulivu na "kujizuia na kuepuka kuzidisha mivutano".

BBC


No comments