FAIZ & BAKSHWEIN, DOUBLE AGENTS WALIOUAWA KIKATILI

 


Miaka kadhaa nyuma baada ya Kenya kupeleka majeshi somalia kupambana na Al shabaab ili kuisaidia serikali iliyokuwa imeelemewa na mzigo huo ndio Al shabaab wakaanza kuingia ndani ya Kenya kufanya mashambulizi kama revenge ya serikali ya Kenya kuingilia na kusaidia serikali iliyopo madarakani somalia.Uwepo wa majeshi ya Kenya ndani ya Somalia iliwa push Al shabaab mbali na kuzima ndoto yao ya kuimiliki somalia yote ndipo Al shabaab wakaanza na kubuni operation mpya ya kuingia Kenya na kufanya mashambulizi kama kumpa message Rais Uhuru ili aondoe majeshi yake Somalia.
Kwenye makundi yote haya kuanzia Al shabaab, Isis,Al Qaeeda kuna informers au double Agents ambao wengi wanaitumikia CIA.Spies hawa hupewa pesa na kila resources ili waweze kufanya kazi kiufanisi na kuwapa taarifa nyeti CIA ili CIA waweze kudhibiti mashambulizi kabla ya kufanyika.
Morten Storm ni jasusi raia wa Denmark ambaye alikuwa anatumikia mashirika 3 ya kijasusi moja wapo ni PET ambayo ni shirika la kijasusi la Denmark ,pili CIA shirika la kijasusi la Marekani na tatu ni MI5 shirika la kijasusi la Uingereza. Morten Storm alitumwa na CIA ajiunge na Al shabaab na ajenge mahusiano na kiongozi wa Al shabaab na pia Mortem alipatiwa pesa na kila dhana na CIA kwa niaba ya mashirika mengine ya kijasusi ili ajenge uaminifu na Viongozi waandamizi wa Al shabaab. Morten Storm akaianza safari yake na ilikuwa mwaka 2008 Storm alianza kutafuta mawasiliano na mtu mmoja aitwaye Ikrima.
2008 Morten alifanikiwa kukutana na Ikrima Nairobi kwa wakati huo Ikrima alikuwa messenger wa Al shabaab tu na Ikrima alikuwa middle man alipokea dhana,vifaa na vitu vingine kutoka kwa Mortem na kumpelekea kiongozi wa Al shabaab kwa wakati huo warsame.Jambo ambalo Ikrima halijui ni kuwa Storm alikuwa jasusi anatumikia mashirika 3 ya kijasusi.Morten storm pia aliweza kumuunganisha Ikrima na Anwar Awlaki kiongozi wa Al Qaeda Yemen ,kabla ya Storm kujiunga Al shabaab alikuwa Al Qaeda na huko alikaa kwa miaka 5 ,Ikrima alikuwa anawasiliana na Awlaki kwa encrypted mails lakini CIA waliweza ku-decrypt encrypted mails hizo na kufuatilia SMS zao.Ikrima alikuwa tayari na heshima na alikuwa strategist wa Al shabaab na ni Storm kwa kiasi kikubwa alimfanya Ikrima awe na status Al shabaab
Kuna watu wanadai WhatsApp ni salama sababu ipo encrypted third party hawezi kusoma hahaa Ikrima alikuwa anatumia encrypted mails lakini CIA walikuwa wana decrypt e mails hizo
Mwaka 2012 Storm alikorofishana na CIA baada ya mission kufanya Yemen Storm na CIA walienda kinyume na makubaliano na hivyo Storm akaachana na CIA na pesa ,dhana ,vifaa vya vita akawapa Al shabaab na September 2012 Al shabaab wakafanya mission ya kushambulia westgate na Storm anaamini Ikrima ambaye alikuwa mtu wake wa karibu alihusika kwenye ku-operate na ku-master mind mission ile.
" Ninahuzunika na kusikitika kwamba Ikrima alihusika na shambulizi la westgate japo sina uhakika ila kwa track ya record yake inawezekana kabisa alihusika.Ninasikitika sana sababu shambulizi hili lingezuilika na ninahuzuni sababu siwezi kuhusika na hili:"-Storm
"Ikrima alikuwa kati ya watu smart sana " Smartest " niliyokutana nao Afrika mashariki
Mr.Storm anasikitika sababu pindi alipokutana na Ikrima kwenye mgahawa Nairobi Ikrima alikuwa Messenger tu lakini baada ya Storm kumpa dhana na vitu Ikrima hapo ndipo Ikrima alijijenga na kujenga status yake ndani ya Al shabaab na akawa kiongozi wa Al shabaab tena wakati huo Ikrima alikuwa na miaka 20 na kitu mdogo tu .CIA plan yao ilikuwa Storm akae karibu sana na Ikrima ili kujua mienendo ya Ikrima na hapo CIA wangepata taarifa nyeti na operations zote za Al shabaab lakini baadae palitokea sintofahamu kati ya Storm na CIA na hivyo Storm akakacha kazi yake mwaka 2012 katikati na mwezi September Al shabaab wakafanya shambulizi westgate..Storm anasema anaamini Ikrima ndiye ali-mastermind kutokana na rekodi yake.
Ikrima anatajwa na CIA kuwa anafahamu lugha 6 kifasaha Kiingereza,Ki-danish,Ki-Norway ,kiswahili,kiarabu na kisomali.
Baada ya shambulizi la westgate mashirika ya kijasusi ya Kenya na marekani wakaanza kupeleka majasusi Al shabaab ili wapate taarifa nyeti na kuzuia planned attacks kabla hazijafanyika.
*_Ahmed Bakshwein._*
- Ahmed Bakshwein ni mfanyabiashara mkubwa wa Lamu na Mombasa ,Ahmed Bakshwein alipata mafunzo yake USA na wabobezi wa mambo wanasema Ahmed Bakshwein ni mtaalamu wa kutumia bunduki na sniper hatari Afrika mashariki na kati.Bakshwein alikuwa jasusi mbobezi na CIA agent na polisi nchini Kenya walimuheshimu sana kama sio kumuogopa na alikuwa anatoa order na mipango kwa polisi.
Ahmed Bakshwein akamtafuta kijana mmoja aitwaye Faiz Mohammed ambaye alikuwa mwalimu wa madrasa malindi na kuanza kumpa mission na mission ilikuwa Faiz aende Al shabaab na ajenge trust na viongozi wa Al shabaab
*_Mr.Faiz former mwalimu wa madrasa na double agent._*
Faiz akaingia rasmi kwenye ujasusi na akawa CIA agent ,Faiz akawa anapatiwa kila kitu fedha za kutosha nk.Faiz akawa ana recruit vijana na kuwapeleka Al shabaab na kitendo hicho Al shabaab wakawa wanamuamini bwana faiz...Faiz alikuwa anasafiri mara kwa mara nchini somalia na alikuwa anapita border bila wasiwasi wowote ule na maofisa na makamanda kwenye Border walikuwa hawambughudhi Faiz ,alikuwa anapewa free pass ..Faiz aliendelea kurecruit vijana na kuwapeleka Al shabaab lengo ni faiz kujenga uaminifu na Al shabaab aonekane yupo nao na ni mtiifu.
Ahmed Bakshwein na faiz waliendelea ku-operate mission yao huku faiz akitumia Mali ya Bakshwein na pesa za CIA kusaidia recruitment ya vijana na mission za Al shabaab.Na bwana Faiz alisaidia kwa Fazzul ambaye alikuwa Al shabaab na msumbufu kukamatwa na maofisa wa kenya hivyo faiz alikuwa anafanya kazi yake kiufasaha
Intelijensia ya Al shabaab ililistuka baadae na wakaweka mtego na mtego huu ulikuwa umewekwa kwa faiz na pasi ya kujua Faiz akaingia kwenye mtego ,ikaandaliwa mission ya kuwa eliminate Faiz na Ahmed Bakshwein ambao walithibitishwa na Al shabaab kuwa ni double agents wanafanyia kazi CIA
Ikatumwa timu ya Hitmen na walienda Malindi na kufanikiwa kumteka Faiz na kumpeleka baharini na kumchinja Faiz na mwili ukabakishwa huku kichwa kikapelekwa Somalia kwa viongozi wa Al shabaab kuthibitisha kama kweli aliuawa .
Mission ya pili ilikuwa kummaliza Jasusi mkubwa Ahmed Bakshwein na Hitmen 3 walipanda bodaboda na kuanza kumfuatilia Ahmed Bakshwein pasi ya Bakshwein kujua kuwa anafuatiliwa na Al shabaab na alikuwa kwenye list ya kuwa eliminated .Ahmed Bakshwein alikuwa kwenye gari lake anaendesha akielekea anapojua mara ghafla pikipiki ilimpita na kwenda kupaki kwa mbele kama mita 15 Bakshwein alikuwa amepaki gari yake pembeni na kama alikuwa anaagiza kitu dukani ndipo jamaa aliyekuwa amepakiwa kwenye bodaboda kushuka na kwenda kumpiga risasi 3,..2 za kifua na moja ya kichwa na Bakshwein alikufa papo hapo na Hitmen walitokomea kusikojulikana..Baada ya Faiz na Ahmed Bakshwein kuwa eliminated Al shabaab wakafanya tukio ndani ya Kenya na kama sijakosea ilikuwa mpeketoni attacks na shambulizi lile lilikuwa successful.
Kifo cha Bakshwein ilikuwa pigo sana kwa serikali ya Kenya na ilitangazwa zawani ya 10Million kwa yeyote ambaye angefanikiwa kusaidia kukamatwa kwa muuaji wa Bakshwein.
Baada ya kifo cha Bakshwein mkewe alifunguka
"Nilikuwa namuona Mme wangu akiongozana na FBI na hata hapa nyumbani walikuwa wanafika na kuzungumza ilikuwa kitambo ila mmoja huwa yuwaja mara nyingi na alikuwa ananiambia nisijitambulishe kwa jina lake nijitambulishe kwa jina lingine lolote alikuwa anahofia ningeweza kupata matatizo...
" Safari zake nyingi alikuwa anafanyia Nairobi na kidogo lamu, kuna nyakati saa nane za usiku alikuwa anapigiwa simu wanazungumza na kiukweli alikuwa na very high intelligence:-" Mkewe Bakshwein
Pia mke wa Faiz alifunguka
Alikuwa yupo pamoja na serikali hio ilikuwa kazi yake siwezi kujua ni kazi gani alikuwa anafanya lkn yeye alikuwa pamoja na serikali pamoja na huyu Ahmed Bakshwein lkn kazi aliyekuwa anaifanya mimi siijui,alikuwa ananiaga anaenda Mombasa kuonana na FBI ila hapa hawajawahi kufika sijawaona wakifika hapa lakini hawa serikali nimewaona hapa wakifika "nyumbani kwake" wakiongea nae ila nilikuwa sijui kipi kinaendelea ":- mke wa Faiz
NB:Unaweza kujiuliza Al shabaab wanapata wapi silaha moja ya source ni kupitia CIA agents ndio wanawapa dhana,vifaa Al shabaab na wanawapa kwa motives zao mfano Mr Morten Storm former CiA na PET agent aliwapatia Al shabaab silaha nk ili awe trusted na awe karibu.
Na pia kuwa double agent ni kucheza na Israeli mtoa roho tumeona namna Faiz na Bakshwein wakiuliwa kikatili Baada ya kugundulika.Pia Taasisi za kijasusi hawalali hupenyeza majasusi ili wazuie mashambulizi na wajui operated zote.
Credit: Facebook story





All reactions:
2

No comments