MIAKA MITATU KM 826 ZA BARABARA ZAJENGWA KIWANGO CHA LAMI
KAGERA
Serikali kupitia Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mkoa wa Kagera imefanikiwa kufungua mtandao wa barabara mpya wa Km. 826 katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kutokana na ongezeko la bajeti.
Mkoa wa Kagera umetengewa bajeti ya fedha shilingi Bilioni 31 mwaka wa fedha 2023/2024 kutoka Bilioni 9 kulinganisha na miaka ya nyuma, jambo ambalo limefanya barabara za mkoa wa Kagera za vijijini kufunguliwa kwa kasi na kurahisisha maendeleo ya wakazi wa mkoa wa Kagera.
Kuongezeka kwa bajeti imeweza kuongeza barabara kiwango cha lami Km 125 kulinganisha na Km 80 za awali, ujenzi wa makalavati 1,600 na kufanya maeneo mengi ya vijijini kupitika kwa urahisi na hivyo kuwezesha wananchi kusafirisha mazao yao sokoni kwa urahisi

Post a Comment