Afisa wa Iran aziambia nchi za Magharibi kuacha kutoa shutuma

 


Tehran imetoa wito kwa mataifa ya Magharibi "kuthamini kujizuia kwa Iran" dhidi ya Israel baada ya kuishambulia nchi hiyo siku ya Jumamosi kulipiza kisasi shambulio baya dhidi ya ubalozi wake mdogo mjini Damascus, Syria.

Iran ilirusha zaidi ya droni 300 na makombora kuelekea Israel lakini takriban 99% ya mashambulizi hayo yalizuiwa, maafisa wa Israel wamesema tangu wakati huo.

"Badala ya kutoa shutuma dhidi ya Iran, nchi [za Magharibi] zinapaswa kujilaumu na kujibu maoni ya umma kwa hatua ambazo zimechukua dhidi ya ... uhalifu wa kivita uliofanywa na Israel" katika vita vyake huko Gaza, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran Nasser Kanani alisema.

Kanani aliongeza kuwa nchi za Magharibi "zinapaswa kufahamu kujizuia kwa Iran katika miezi ya hivi karibuni".

BBC

No comments