Extra Bongo yatua Songea, kuburudisha La Chaz
KIONGOZI wa bendi ya muziki wa dansi ya Extra Bongo, Ally Choki, amewasili mjini Songea mkoani Ruvuma akiwinda kufanya maonyesho kadhaa ya burudani katika ukumbi maarufu wa baa ya La Chaz iliyopo mjini humo.
Akizungumza kwaq njia ya simu jana na Ojuku Blog akiwa Songea, Choki maarufu kama Mzee wa Farasi, alisema amefika mjini humo kwa ajili ya kufanya mazungumzo ya kazi na mmiliki wa ukumbi huo, moja kati ya maeneo ya starehe yenye mashabiki wengi.
"Bado sijaanza kufanya maonyesho, lakini nilizungumza na mmiliki wa La Chaaz ambaye ndiye amenileta hapa ili tuweze kufanya mazungumzo ya kuona ni kwa namna gani tunaweza kufanya kazi pamoja. Mambo yakiwa vizuri nitakufahamisha," alisema Choki.
Hata hivyo, nyota kiongozi huyo wa zamani wa bendi za African Stars 'Twanga Pepeta na Nchinga Sound, hakuweka wazi kama amekwenda huko akiwa na kundi lake kamili au la.
Extra Bongo ambayo hii ni mara yake ya tatu ikijiunda upya, inao wanamuziki kadhaa nyota hivi sasa wakiwemo Bob Kissa na Rama Pentagon, ambao pia wamewahi kuhudumu katika kikosi hicho siku za nyuma.

Post a Comment