WANANCHI WA TUNDURU WAISHUKURU SERIKALI KWA KUBORESHA UPATIKANAJI WA HUDUMA BORA ZA AFYA

 


Wananchi wa Wilaya ya Tunduru wameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kuboresha mazingira ya utoaji wa huduma za afya katika hospitali ya Wilaya, huduma ambazo hapo awali walilazimika kuzifuata nje ya Wilaya ya Tunduru.

Hospitali ya Wilaya ya Tunduru imepata mabadiliko makubwa baada ya kukarabatiwa, Ukarabati huu umesaidia kuboresha huduma za afya na kuleta ahueni kubwa kwa wananchi wa wilaya ya Tunduru, ambao sasa wanaweza kupata huduma bora za afya karibu na makazi yao. 

Fedha kiasi cha shilingi milioni 900 zilizotengwa na serikali ya awamu ya sita zimetumika vizuri katika kuboresha miundombinu ya hospitali, vifaa vya tiba, na mazingira kwa ujumla.

Ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje (OPD) na Maabara pamoja na ukarabati wa jengo la upasuaji umekamilika na majengo haya yanatumika. Maabara imekarabatiwa na sasa ina vifaa vya kisasa vinavyowezesha vipimo sahihi na utambuzi wa magonjwa kwa ufanisi Zaidi, Jengo la upasuaji linatoa huduma katika mazingira safi na salama kwa ajili ya upasuaji na pia Hospitali ina vifaa vya kisasa vya tiba, na vifaa vya kufuatilia afya ya wagonjwa.

Kama alivyosema Mganga Mkuu wa Wilaya wa Hospitali ya Tunduru, Dk.Wilfred Rwechungura, "Kukamilika kwa mradi huu kumepunguza changamoto kubwa ya uchakavu wa miundombinu katika Hospitali na pia kusaidia kumehisisha utoaji wa huduma bora za afya kwa wananchi wa wilaya ya Tunduru."

Wananchi wamefurahishwa na juhudi za Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania za kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma bora na kwa wakati ili kuokoa maisha ya watanzania.

No comments