BALOZI NCHIMBI AKOSHWA NA MAFUNZO YA VIONGOZI WA KISIASA WANAWAKE NCHINI.

 

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi amefurahishwa na mafunzo yanayotolewa kwa Viongozi wa kisiasa wanawake nchini yanayoratibiwa na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT).

Balozi Dkt. Nchimbi amesema kuwa mafunzo hayo yanaenda kuwaongezea uwezo viongozi wa kisiasa wanawake.

“Ni wazi mafunzo haya yanakwenda kuongeza uwezo katika shughuli zenu za kisiasa ambazo zinakwenda kukiimarisha chama chetu cha CCM na taifa letu kwa ujumla”Alisema Dkt. Nchimbi na kuongeza

“Nitoe pongezi kwa Mwenyekiti wa UWT Taifa Mama yetu Ndg. Mary Pius Chatanda kwa kazi kubwa anayoifanya kuanzia kwenye kuratibu mafunzo haya na shughuli zingine zinazoimarisha jumuiya ya UWT na chama chetu cha CCM”

Dkt. Nchimbi ameyasema hayo jana Aprili 9, 2024 wakati wa mafunzo kwa viongozi wa kisiasa wanawake yaliyofanyika katika ukumbi wa NEC-Dodoma.


No comments