Shilingi 22,950,000 zachangishwa kwa ajili ya waathirika wa mafuriko Rufiji

Mwenyekiti chama cha mapinduzi mkoa wa Dar es salaam ndugu ABASI MTEMVU akiwa na Mjumbe wa halmashauri kuu ya Chama cha mapinduzi taifa kutokea mkoa wa Dar es salaam ndugu JUMA SIMBA GADDAFY na wajumbe wa kamati ya siasa ya mkoa wa Dar es salaam  wameongoza harambee kwaajiri ya  waathirika wa janga la mafuriko mkoa wa pwani Wilaya ya Rufiji 

Katika harambee hiyo kiasi cha shilingi milioni Ishirini na mbili na laki tisa zimekusanywa ili kuwasaidia waathirika wa Mafuriko yaliyotokea hivi karibuni huko Rufiji. 

Akiongea na vyombo vya habari Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Dar es salaam ABBAS MTEMVU amesema fedha hizo zimechangwa na  wadau na viongozi mbalimbali akiwepo Naibu Spika wa Bunge la Tanzania MUSA ZUNGU ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ilala ametoa Pesa taslim milion moja na maji katoni 500 kutoka kampuni ya Uhai Watu Wengine walio fanikiwa kuchangia ni Mjumbe wa kamati ya Siasa Mkoa wa Dar es salaam ambaye ni Mkurugenzi wa Chuo cha City Collage ABUBAKAR BOKA ametoa Pesa taslim milion tatu , kampuni ya Big Bon Milioni tano Oil Com wametoa milion kumi, na OBASANJO ametoa Milioni Moja.

Ameongeza pia mahitaji mengine yaliyooletwa ni Magodoro, unga, Maharagwe, n a mahitaji mengine yaliyotolewa na TOSH LOGOSTIC pamoja na AMO FOUNDATION Chini ya mkurugenzi wake AMINA SAID GOOD wametoa Unga wa Sembe  Tani  Moja Na Maharagwe Tani Tatu.

Aidha Mwenyekiti MTEMVU ameeleza michango mingine imetolewa na viongozi wa Chama ngazi ya kata na baadhi ya madiwani wanaopatika mkoa wa Dar es salaam na wadau mbalimbali imepokelewa wao wamechanga kiasi cha milion mbili na bado wanaendelea kuchanga.

Kufuatia Kupokelewa kwa mahitaji hayo ameendelea kutoa wito kwa wananchi na wanachama kujitokeza katika ofisi za CCM Mkoa wa Dar es salaam kutoa michango yao.


No comments