TUPANDENI MITI KWA WINGI NA KUFUATILIA UKUAJI WAKE

 


Na Dk.Mwampogwa-Tanga

Binadamu na hata Wanyama wa kufugwa na waishio majini na misituni ni kawaida yao kuzaa na kutunza Watoto wao mpaka wahakikishe wanaweza kujitegemea kwa kutembea,kujitafutia Chakula na kuishi wenyewe bila kuhitaji msaada.

Ni vyema katika kampeni ya Upandaji Miti kwa ajili ya Utunzaji wa Mazingira ambayo inaendelea nchini tukahakikisha sisi tunaopanda Miti hiyo baadae tuendelee kufuatilia ukuaji wake kwa kuipa mahitaji muhimu kama Maji,Mbolea nk kuliko kupanda miti mingi bila ya kuwekeza uangalizi wake.

Hata katika hali ya kawaida sisi tungezaliwa na kuachwa bila huduma yoyote kutoka kwa Wazazi wetu,Walezi wetu au Watu wetu wa karibu tusingeweza kubaki hai mpaka sasa hivi.

Kampeni ya Utunzaji wa Mazingira yetu ni muhimu sana na inamgusa kila mtu katika taifa letu.Ni jukumu la kila mmoja kwa nafasi yake kutoa Elimu kwa Jamii,kuhamasisha na kuonyesha kwa Vitendo namna ya kutunza Mazingira.

Madhara ya uharibifu wa Mazingira yetu hususan Misitu ni hatari kwa taifa letu.Tatizo la madhara ya uharibifu wa mazingira linaanza taratibu na suluhu yake haiwezi kupatikana kwa muda mfupi.Wananchi Mifugo na Mazao nk vitakuwa hatarini sana iwapo mazingira ya nchi yataharibiwa.

📌

USHAURI.


Serikali yafaa ipitie Upya Sheria inayohusiana na Mazingira.Mfumo mzuri ambao unamgusa kila Mwananchi kuwajibikia mazingira ya nchi yake uwekwe na pia Utunzaji wa mazingira liwe suala ambalo halina chaguo kwa kila Mwananchi.

Viongozi wetu ambao wanasimamia Mazingira na Misitu katika maeneo yote nchini yafaa waendelee ku-set mpango nzuri wa kutoa Elimu kwa Wananchi ikiwa ni pamoja na kuwahamasisha Wananchi kupanda miti,kuitunza na kutunza Mazingira yote kwa ujumla ikiwemo vyanzo vya Maji.

Katika kila Kijiji au Mtaa kuna Kamati tatu;- (1)Kamati ya Mipango Uchumi na fedha (2)Kamati ya Huduma za Jamii (3)Kamati ya Ulinzi na Usalama.Binafsi nashauri Wajumbe wa Kamati hizi wawezeshwe kimafunzo wanaweza kusaidia Ulinzi na Usalama wa Misitu,Vyanzo vya Maji na mazingira yetu kwa ujumla.

Sheria ichukue mkondo wake tena bila huruma kwa Wale wote ambao wataharifu katika suala zima la Utunzaji wa Mazingira yetu.

Miti iwe ya Matunda, Mbao na Kivuli ipandwe kwa mipango endelevu au utaratibu maalum kwani tusipo angalia tunaweza kwenda kupanda miti ya kivuli Shambani na miti ya matunda na mbao tukaijaza Mjini hali ambayo baadae inaweza kuwa changamoto.

Viongozi wanao simamia mazingira waweke U-serious katika Viwanda kujua Takataka ngumu, nyepesi na kimiminika zinazotoka katika Viwanda hivyo zinahifadhiwa au kuteketezwa katika maeneo sahihi ili kuepuka kuleta madhara kwa Wananchi mfano Maji yenye Kemikali kuchanganyika na Maji safi na salama yanayotumiwa na Wananchi huweza kusababisha Saratani au Magonjwa ya tumbo na Ngozi kwa Wananchi.

Matumizi ya Nishati ya Gesi,Umeme na 'Majiko okoa misitu' katika kupikia ni jambo jema sana ambalo huweza kupunguza Matumizi ya Nishati ya Kuni na Mkaa katika taifa letu.

Lakini tukirudi katika namna ya Uzalishaji wa Miche ya Miti nadhani Shule zetu za Msingi na Sekondari zinaweza kuwezeshwa kwa Elimu na Vifaa nazo zikawa sehemu ya kuandaa Vitalu vya Miti ya Matunda,Mbao na kivuli na kuweza kusaidiana na vyanzo vingine vya Uzalishaji wa Miche ya Miti lengo hapa ni kupigania Tanzania ya Kijani kwa kumsaidia Mhe.Rais wetu kutimiza maono yake ambayo ndiyo maono ya taifa letu.

Kongole za dhati zimwendee Mhe.Rais wetu Dk.Samia Suluhu Hassan,Chama tawala na Serikali yetu kwa Kazi kubwa na nzuri inayo endelea nchini katika eneo hili la Utunzaji wa Mazingira yetu.


📌

Karibuni sana Tanga Jiji.

S/msingi Duga Kata ya Duga.

Simu Na. 0628414250 au 0679404150

No comments