Kocha Simba: Al Ahyl timu bora inakutana na Simba ngumu
Al Ahly ni timu namba (1) Africa kwa ubora
Al Ahly ni timu namba (1) Africa kwa mafanikio pamoja uwekezaji
Al Ahly ni timu namba (1) Africa wenye wachezaji ghari zaidi ...
Lakini japo wao ni bora zaidi yetu katika mambo mengi ila tunaomba kuwaambia kuwa tunakutana timu tofauti hii tunasema zinakutana timu bora na timu ngumu...
Kwangu kama kocha jeshi langu mpaka sasa liko sawa Kwa mapambano Al Ahly kwangu sio timu ngeni kwa sababu mwaka jana tumekutana katika final ya kombe la super cup nikiwa na timu ya Mc Alger ya Algeria na kufanikiwa kuwafunga na kutwaa ubingwa pia hata mwenye timu yangu ya sasa Al Ahly sio timu ngeni sababu record zinaonyesha mara ya mwisho kukutana ilikuwa mwaka jana katika Africa super league na kutoshana nguvu kwa kutoa sare mechi zote mbili ...
Hivyo niwaondoe wasiwasi kuwa tunaenda kupambana na tutapambana na tutashinda na sio kushinda tutafanikiwa kuingia nusu huu mwaka sio mwaka wa makosa tena 💪

Post a Comment