Rais Samia, Mbowe wamzungumzia Lowassa wa Chadema

Wakati viongozi wengi wa serikali na Chama Cha Mapinduzi na vyombo vya habari vya serikali vimeacha kumzungumzia marehemu Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kuhudumu chama cha upinzani, Rais Samia na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe wamevunja mwiko huo.

Katika salamu zake za pole kwa familia na Taifa, Rais Samia alisema pamoja na mambo mengine, Lowassa alikuwa mfano bora wa mwanasiasa aliyejenga demokrasia, kwani licha ya kuhama kwake CCM kwenda Chadema, hakuwahi kukisema vibaya chama hicho wala viongozi wake.

Aidha, Rais Samia alisema hata baada ya kurejea chama chake cha awali, bado Lowassa hakuwahi kuisema vibaya Chadema wala viongozi wake.

Kwa upande wake, Mbowe alisema hata kama wasifu wa Lowassa utasomeka vile wanavyotaka, bado ukweli kwamba kiongozi huyo alihudumu Chadema akiwa mjumbe wa Kamati Kuu kwa kipindi cha miaka minne haiwezi futika.

Waziri Mkuu wa zamani Lowassa amezikwa leo nyumbani kwake Monduli.

No comments