Raheem Sterling akataa ofa ya mshahara wa bilioni 2.8 Saudia

Raheem Sterling, nyota wa kimataifa wa England, amekataa ofa ya kulipwa mshahara wa shilingi bilioni 2.8 kwa wiki katika Ligi Kuu ya Saudi Arabia.

Sterling ambaye kwa sasa yupo London akikipiga na Chelsea, anasemekana kulipwa dola 300,000 kwa wiki, sawa na shilingi za kitanzania milioni 985.

Timu iliyomtaka, ambayo haijatajwa, ilikua tayari kumlipa mshahara mara tatu ya sasa.

Endapo nyota huyo wa zamani wa Man City angekubali kuungana na nyota wengine katika ligi hiyo ya kiarabu akiwemo Cristiano Ronaldo, Neymar Jr, Karim Benzema na Saido Mane, inadaiwa angekuwa mchezaji wa tatu kwa kulipwa pesa nyingi katika ligi hiyo.

No comments