Mzee Lowassa: Kimya Milele
Hatimaye, Waziri Mkuu wa zamani, Edward Ngoyai Lowassa amepumzishwa katika nyumba yake ambako atabakia kimya milele.
Katika hali ya upendo mkubwa, Watanzania wote, bila kujali itikadi, dini wala ukabila, waliungana pamoja kuanzia ugonjwa, kifo chake hadi mazishi yake leo nyumbani kwake Monduli.
Kwa hisia tofauti, kila mmoja alimuelezea mzee Lowassa kama mwanasiasa mvumilivu, mnyenyekevu, mkweli na mpenda demokrasia ambaye katika uhai wake, alifanya kila aliloweza kuifanya Tanzania kuwa salama kuishi.
Mamia ya waombolezaji wa makundi mbalimbali, waliujaza mji wa Monduli, wakitoka kila pembe ya nchi, wakiwemo wanasiasa, wasanii, viongozi wa dini zote na wananchi wa kawaida.
Rest In Peace E. N. L

Post a Comment