Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Prof. Godius Kahyrara amesema Serikali
ya Jamhuri ya Tanzania kwa kushirikiana Serikali ya China inatarajia
kuliboresha Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (TARAZA) ili kuliwezesha
kuongeza ufanisi hususani katika usafirishaji wa mizigo.
Prof. Kahyrara ameyasema hayo jijini Dodoma wakati aaliposaini mkataba wa
Utendaji kazi na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) na
kusisitiza kuwa tija ya maboresho hayo ni pamoja na kukuza pato pato la taifa
na urahisi kwenye usafirishaji wa mzigo kutoka eneo moja kwenda jingine.
“Shirika la TAZARA ni moja ya mashirika ambayo yanapewa kipaumbele kwa
sasa hasa katika uboreshaji wa miundombinu ambayo kwa muda mrefu
haikukarabatiwa na wenzetu wa Serikali ya China wameonyesha nia ya kusaidia
kwenye eneo hilo” amesema Prof. Kahyrara.
Katibu Mkuu Prof. Kahyrara amesema tayari Serikali imefanya maboresho
katika Sheria ya Reli ili kuruhusu sekta binafsi kutoa huduma katika Reli ya
TAZARA na TRC.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa TRC Bw. Masanja Kadogosa amesema
miradi mbalimbali inaendelea kutekelezwa kwa reli ya Kati na Reli ya Kisasa
ambayo hivi karibuni majaribio yatafanywa na kuanza kutoa huduma.
Mkurugenzi Kadogosa ameongeza kuwa vitendea kazi kwa ajili ya uendeshaji
wa SGR vimeendelea kuwasilia ambapo hivi karibuni TRC imepokea Kichwa
kimoja cha reli hiyo kutoka Korea kusini ambapo kichwa hicho ni miongoni
mwa Vichwa kumi na Saba ambavyo vimeagizwa.
Naye Mkurugenzi wa Tathimini na Ufutiliaji kutoka Wizara ya Uchukuzi Bi.
Devota Gabriel amemuhakikishia Katibu Mkuu Prof. Kahyarara kuwa kitengo
hicho kimewekea mikakati thabiti itakayowezesha wataalam wa Wizara
kusimamia kwa karibu miradi iliyopangwa kutekelezwa kwa mwaka wa fedha
2023/2024 ili kuzingatia thamani na ubora.
(Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Uchukuzi)
Post a Comment