ASAMOH GYAN AAMRIWA KUMLIPA MKEWE NYUMBA MBILI, KITUO CHA MAFUTA NA MAGARI MAWILI
Nahodha wa zamani wa timu ya Taifa ya Ghana, Asamoh Gyan ameamriwa na mahakama kumlipa mke wake wa zamani, baada ya kuwa wapo katika mzozo wa kindoa kwa zaidi ya miaka mitatu sasa.
Awali, Gyan alidai watoto watatu aliozaa na mwanamke huyo hawakuwa wanaye wa damu, lakini vipimo vya kinasaba vilithibitisha kuwa ni watoto wake na hivyo kutakiwa kumlipa mwanamke huyo aliyekuwa akiwalea watoo hao peke yake nyumba mbili zilizopo Uingereza na Ghana, kituo cha mafuta na magari mawili, ambavyo ni baadhi ya mali anazomiliki mwanasoka huyo.

Post a Comment