Jeshi la Israel lasema Hamas imepoteza 'makumi' ya wapiganaji katika makabiliano ya usiku kucha

 


Vikosi vya Ulinzi vya Israel, IDF, vimeripoti mapigano makali kati yao na Hamas katika Ukanda wa Gaza usiku kucha na kudai "makumi" ya vifo vya wapiganaji upande wa Hamas.

IDF ilisema Hamas ilirusha makombora ya kukinga vifaru, kulipua vilipuzi na kurusha guruneti kwa vikosi vya Israel

Ilisema ilijibu kwa mizinga, shambulio la angani kutoka kwa helikopta na shambulio la kombora kutoka kwa boti ya jeshi la wanamaji.

IDF pia iliripoti mapigano ya ardhini kati ya wanajeshi wake na Hamas.

Wakati huo huo waziri wa ulinzi wa Israel Yoav Gallant anasema jeshi la Israel limedondosha zaidi ya mabomu 10,000 kwenye mji wa Gaza pekee tangu kuanza kwa mzozo wa sasa na inaendeleza lengo lake la kuwamaliza Hamas.

Zaidi ya watu 400 waliokuwa wamenaswa huko Gaza, wakiwemo baadhi ya raia wa Uingereza na wengine wa kigeni, sasa wamevuka mpaka kuingia Misri

Kivuko cha Rafaa kinatarajiwa kufunguliwa tena baadaye leo ili kuruhusu watu zaidi kuondoka katika eneo hilo.

No comments