HOSPITALI GAZA KUSITISHA HUDUMA, MAFUTA YATAISHA LEO

 


Wakati mashambulizi ya anga kutoka kwa jeshi la Israel yakiendelea kuupiga mji wa Gaza, maofisa wa Umoja wa Mataifa wamesema Hospitali ya Nasser huko Khan Younis, itasitisha kutoa huduma ya kuokoa maisha ya watu kutokana na kuishiwa viifaa.

Inadaiwa kuwa dawa, damu na maji vimeisha na upatikanaji wa vitu hivyo ni wa kiwango cha chini mno, huku akina mama na watoto wakiwa ndiyo wahanga wakubwa.

Zaidi ya watu milioni moja wanadaiwa kuyakimbia makazi yao huko Gaza, wakiwa ni nusu ya idadi ya watu wa eneo hilo na wengi wamekimbilia kulala hospitalini na mashuleni kuogopa mashambulizi.

    Katika shule moja huko Gaza, mwandishi wa BBC alishuhudia idadi ya watu elfu tano wakiwa wamejihifadhi shuleni hapo, katika eneo ambalo awali lilimudu kuhifadhi watoto 500 tu.

Watu hao wamekuwa wakipewa lita moja ya maji kwa siku na chakula kidogo na mlundikano unawafanya washindwe kupumua. 

No comments