KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MIUNDOMBINU YAITAKA KAMPUNI YA HUDUMA ZA MELI (MSCL) KUJIENDESHA KIBIASHARA.

 




Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imeitaka kampuni ya
Huduma za Meli (MSCL), kuhakikisha meli zote za kampuni hiyo zinafanya
kazi na kujiendesha kibiashara .
Hayo yamesema na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mheshimiwa Selemani
Kakoso kwenye Kikao cha kupokea taarifa za utendaji kazi ya kampuni
hiyo kwa kipindi cha Julai- Oktoba 2023.
“MSCL inatakiwa kuhakikisha inakarabati Meli zote na kusimamia meli
zilizopo katika Ziwa Tanganyika, Ziwa nyasa na Ziwa Victoria na
Mjiendeshe kibiashara” alisema Kakoso.
Pia Kakoso ameongeza kwa kusema kuwa katika bajeti ya Mwaka
2022/2023 MSCL ilitengewa shilingi Bilioni 124 hivyo kamati hiyo
inamatumaini itasaidia Kampuni hiyo kuweza kukarabati na kujenga meli
Mpya ili kuweza kutoa huduma ya Usafiri kwa Njia ya Maji.
Kwa Upande wake Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile amesema
kuwa Serikali inaendelea kuboresha huduma kwa njia ya Maji katika Ziwa
Tanganyika na Ziwa Victoria na Tayari Serikali imeshawezesha kusainiwa
mikataba ya Ujenzi wa Meli mbili za Mizigo pamoja na Kiwanda cha
kutengeneza Meli katika ziwa Tanganyika.
Serikali pamoja na kutoa fedha ya Ujenzi wa Meli Mpya mbili lakini pia
serikali imetoa fedha ya ukarabati wa meli ya MV. Umoja, MV.Liemba na
MV. Muongozo” alisema Kihenzile.
Mkurugenzi wa MSCL Erick Hamis amesema kuwa Ujenzi wa Meli ya
MV.Mwanza hapa kazi tu inatarajia kukamilika Mwezi Mei mwaka huu
kwani hatua iliyofikia sasa ni uwekaji wa viti na Vitanda, na vitu vyote
kama Mashine na Mitambo vimekamilika.
MSCL inajumla ya meli 18 kati ya meli hizo meli saba tu ndio zinafanya
kazi hivyo Kampuni hiyo inaendelea kusimamia na kuendesha meli hizo
katika Ziwa Nyasa,Ziwa Tanganyika na Victoria

No comments