DEREVA WA TRENI KUADHIBIWA KWA KWENDA KUJISAIDIA

DEREVA wa Treni iliyobeba Watu 160 Nchini Japan, anakabiliwa
na adhabu baada ya kuachia nafasi yake kwa dakika kadhaa ili kwenda kujisaidia
Dereva huyo wa miaka 36 aliumwa tumbo na alihitaji kwenda
Maliwatoni haraka hivyo alimwita Kondakta asiye na Leseni ya Udereva, na
kumwachia Treni kwa dakika tatu. Wote wawili wanakabiliwa na adhabu
Reli za Japan zinasimamiwa kwa viwango vya juu vya usalama na
mara ya mwisho ajali kubwa kutokea ilikuwa mwaka 2005 ambapo watu 107
walifariki dunia.

Post a Comment