Kamati ya siasa na Uchumi Pwani yatoa fedha kwa wahanga wa mafuriko Kibiti, Rufiji


Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani chini ya  Mwenyekiti wake Ndg. *MWINSHEHE MLAO* pamoja na Kamati ya Uchumi ya Mkoa wamewatembelea Wahanga wa Mafuriko katika Wilaya za Rufiji na Kibiti na kutoa fedha taslimu shilingi Milioni 18.

Fedha hizo zimetolewa kwa ajili ya kununua mafuta ya magari na boti ili kufanikisha zoezi la usambazaji wa vyakula na mahitaji mengine katika Kambi za Wahanga hao.

Akitoa taarifa ya Serikali Mkuu wa Mkoa wa Pwani *Alhaji Abubakari Kunenge*  amesema Wadau na Taasisi mbalimbali wameendelea kutoa misaada kwa Waathirika wa Mafuriko.

Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Pwani imemshukuru na Kumpongeza *Mhe* , *Daktari Samia Suluhu* *Hassan* Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kwa moyo wake wa kizalendo wa kuwa karibu na wananchi pindi wanapopatwa matatizo.

Aidha Kamati hiyo, imemshukuru *Alhaji Abubakari Kunenge* Mkuu wa Mkoa wa Pwani kwa Jitihada zake za kutafuta Wadau kwa ajili ya Kuwasaidia Waathirika hao.


*#Jambo la Kibiti na Rufiji ni letu sote*.

*#ahsante Samia*

*#ahsante Kunenge*


Imetolewa na: 

David Mramba 

Katibu wa Siasa, Uenezi na Mafunzo CCM Mkoa wa Pwani,

*KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI*

No comments