YESU WA KENYA AKIMBILIA POLISI AKIHOFIA KUSULUBISHWA MSALABANI
Eliud Wekesa ambaye amejizolea umaarufu mkubwa katika miezi ya karibuni baada ya kujitangaza kuwa yeye ni Yesu halisi aliyerudi duniani, amekimbilia Polisi baada ya wakosoaji wake kumtaarifu kuwa watamsulubu msalabani wakati wa Pasaka ili afufuke siku ya tatu kama ilivyokiwa kwa Yesu wa Nazareti.
Wekesa anajiita Yesu wa Tongoren akitokea Bungoma, aliwaambia polisi kuwa maisha yake yapo hatarini, kwani sasa ni dhahiri kuna watu wanajiandaa kumsulubu msalabani wakati wa kipindi cha pasaka kinachokuja.
Kiongozi huyo wa dini, ambaye amekuwa akihubiri kwa kumuiga Yesu, amekuwa akidai kuwa yeye ndiye Yesu halisi aliyerejea duniani, baada ya kupaa siku tatu tangu asulubiwe hadi kufa msalabani kwa hukumu ya uonevu kutoka kwa Waisrael zaidi ya miaka 2000 iliyopita.

Post a Comment