MBELGIJI APEWA MIKOBA TAIFA STARS

Shirikisho la Soka Nchini TFF limemtangaza kocha mpya, raia wa Ubelgiji, Adel Amrouche kuinoa Timu ya Kandanda ya Tanzania, Taifa Stars.

Taarifa ya shirikisho hilo iliyotolewa na kusainiwa na Ofisa Habari wake, Cliford Ndimbo, imesema Amrouche, mwenye asili ya Algeria amewahi kuzifundisha timu kadhaa za Afrika zikiwemo Kenya, Guinea ya Ikweta, Botswana, Libya na Yemen.

Kwa upande wa klabu, taarifa hiyo imesema kocha huyo amewahi kufanya kazi na timu za USM Alger, RC Kouba na MC Algiers.

No comments