RAIS SAMIA SULUHU HASSAN MGENI RASMI MKUTANO WA CHADEMA

Ni kama hadithi, lakini ni kweli.

Katika hali ambayo haijawahi kushuhudiwa, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, Rais Samia Suluhu Hassan, amekubali kuwa mgeni rasmi katika mkutano wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani, ambao umeandaliwa na Baraza la Wanawake la Chadema.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ambaye mwishoni mwa wiki alikutana na Rais Samia katika ikulu ndogo ya Arusha, ametoa kauli hiyo jana akisema mama amekubali mwaliko na yeye Mbowe atakuwepo kumpokea.

Hili ni jambo jema kwa siasa za Tanzania katika miaka hii ya demokrasia

No comments