XI JIMPING ATEULIWA TENA URAIS CHINA

Rais Xi Jimping ambaye ameiongoza China kwa muongo mmoja uliopita, amechaguliwa tena kuwa kiongozi wa nchi hiyo, sambamba na Kamati Kuu ya Chama Cha Kikomunisti.

Kabla ya Jimping, ni Rais Mao pekee ndiye alitawala kwa muda mrefu na baada ya kifo chake, uliwekwa ukomo wa vipindi viwili vya uongozi ambavyo viliondolewa na Xi mwaka 2018.

Katika muhula wake wa tatu wa miaka mitano mitano, Rais Xi anategemewa kuteua mawaziri ambao watakuwa watiifu kwake, akiwa pia ndiye Amiri Jeshi Mkuu wa Jeshi la Watu wa China.

No comments