CHEICKNA DIAKITE BADO AITOA UDENDA YANGA
Winga tereza wa Real Bamako ya Mali ambaye alionekana kuisumbua ngome ya Yanga katika mechi zote mbili za Kombe la Shirikisho, Cheickna Diakite bado anawavutia vigogo hao wa Jangwani.
Habari kutoka vyanzo vya ndani ya klabu hiyo iliyo chini ya mabosi wa GSM, zinasema wanajipanga kumchukua kijana huyo mwenye umri wa miaka 18, ambaye viongozi wake wanasema wana ofa nyingi kutoka Ulaya.
Klabu hiyo ya Mali inasema winga wake anazivutia timu nyingi za Ulaya siyo tu kwa sababu ya uwezo wake, bali pia umri wake kwani atacheza kwa muda mrefu.
Huo ni mtego wa kutaka kupata fedha nyingi toka Jangwani.

Post a Comment