DAR ES SALAAM: WASHAMBA WENGI KULIKO MIJI YOTE TANZANIA

Kwa mujibu wa sensa ya mwaka jana, Jiji la Dar ea Salaam lina wakazi wapatao milioni sita, wengi kuliko mji mwingine wowote katika Tanzania.

Licha ya idadi hiyo kubwa ya watu, lakini pia ni jiji linalokua kwa kasi miongoni mwa majiji yaliyo kusini mwa jangwa la sahara.


Kwa Tanzania, ndilo jiji linalopokea wageni wengi kuliko mji wowote kwa siku, wakiiingia kupitia usafiri wa mabasi, treni, meli, boti, ndege, malori na magari madogo.

Inakadiriwa zaidi ya mabasi ya abiria 300 huondoka na kuingia kila siku katika Kituo Kikuu cha Mabasi cha Magufuli (Magufuli Terminal) kilichopo Mbezi , ukiachana na mabasi mengine yanayoanza safari zake kuanzia maeneo mbalimbali ya jiji.


Inaaminuka kuwa jiji la Dar es Salaam ndilo makazi ya watoto wa mjini kwa maana ya wajanja wa mipango. Hili halina ubishi hata kidogo kwani simulizi za kuthibitisha ukweli huu zipo nyingi.

Hata hivyo, si wengi wanafikiri kwamba Dar es Salaam pia ndipo nyumbani pa washamba wengi (watu mbumbumbu, wasiojua kitu na malimbukeni).

Kuwatambua watu hawa ni rahisi zaidi kama utakuwa katika maeneo yenye mikusanyiko ya watu wengi kama Kariakoo, Feri, minadani, masokoni, stendi na mahospitalini.


Moja kati ya njia rahisi za kuwatambua washamba wa jiji, ni jinsi unavyoweza kumuona mtu ambaye kwa kumwangalia tu unamjua kuwa hajui, lakini mbele za watu atajifanya anajua.

Anaongea sana, anajua kila kitu! 

Lakini pia lafudhi. Watu wa Dar wana lafudhi yao, wanaojaribu kuiga wanafahamika. Mtu mjanja hawezi kuiga lafudhi, ataongea lafudhi yake lakini haumdanganyi.

Lakini pia washamba hawa utawakuta wakiendesha bodaboda, wakiwa makondakta na madereva wa daladala, au madereva teksi. Kwa kuwa anaambiwa Dar es Salaam madereva wanatanua, basi atataka kutanua bila hata kutumia akili.





No comments