WEZI WAMUIBIA KILEMA MALI ZA MILIONI 100

 


Kijana Aidan Beltran ambaye ni mlemavu wa mwili, mwenye umri wa miaka 15, ameibiwa vifaa vyake vyenye thamani ya dola za Marekani 50,000 sawa na fedha za Kitanzania zaidi ya shilingi milioni 100.

Mama yake, Alicia Rodriguez alisema kijana wake huyo aliibiwa baiskeli iliyotengenezwa maalum kwa ajili yake na kiti chake cha kukalia kwenye gari, ambavyo vyote vina thamani hiyo.


Tukio hilo lilitokea huko Illinois nchini Marekani ambapo kiti hicho maalum kina thamani ya dola 30,000 karibu shilingi milioni 70 na kiti cha gari kikiwa na thamani ya dola 19,000 sawa na shilingi milioni 40.

Alicia ambaye hana mume, amesema vifaa hivyo vilikuwa ni muhimu kwa mwanae ili aweze kuwahi miadi ya madaktari wake ambao wamekuwa wakimtibu kwa muda wote kutokana na kupooza.

No comments