JOHN TRAVOLTA, MUIGIZAJI MWENYE NDEGE SABA BINAFSI, IPO BOMBARDIER NA BOEING

 

Muigizaji John Travolta anaweza kuwa na vituko vingi unavyovifahamu, lakini kitu ambacho kinaweza kukushangaza ni jinsi alivyoweza kutoka kuwa mtu wa kawaida kabisa, aliyesoma Buchannan High School  hadi kuwa mtu anayemiliki ndege kadhaa.

Akiwa ni mmoja kati ya waigizaji wa muda mrefu na aliyefanikiwa zaidi nchini Marekani, John Travolta licha ya kuwa na fedha za kutosha katika akaunti yake, lakini pia ni mmiliki wa ndege binafsi karibu saba.

Na kwa wasiofahamu ni kwamba muigizaji huyu pia ni rubani aliyesomea kurusha ndege. Baadhi ya ndege anazomiliki ni aina za Boeing 707, Bombardier Challenger 601, Boeing 727 na Gulfstream nne.

No comments