MSCL YAAGIZWA KUTAFUTA MASOKO

 

Kamati ya kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) imemtaka

Mwenyekiti wa bodi ya Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) kuhakikisha kitengo

cha   masoko   kinaanza   kutafuta   kampuni   za   kusafirisha   mzigo   kwenye   meli

zinazojengwa na kufanyiwa ukarabati ili kuziwezesha meli hizo kuanza kazi mara

moja baada ya ujenzi na ukarabati kukamilika.

Akizungumza mkoani Kigoma mara baada ya kukagua mradi wa ukarabati wa meli ya

MT. Sangara na eneo ambalo litajengwa chelezo kipya Mhe. Jerry Silaa amesema

uwekezaji wa fedha uliowekwa hususani kwenye miradi ya ujenzi na ukarabati wa

meli   unawapa   jukumu   kampuni   hiyo   kuhakikisha   wanapata   mzigo   wa   uhakika

utakaowawezesha kupata fedha na hatimaye kuanza kujilipa mishahara na kuendesha

kampuni bila kutegemea fedha kutoka Serikalini.


“Serikali imeshaweka fedha nyingi kwenye kampuni hii, na kamati yetu ina jukumu la

kuhakikisha   mnapata   fedha   za   kuweza   kujiendesha   wenyewe   pasipo   kutegemea

ruzuku kutoka Serikalini, mtafanikiwa kupata fedha mtaanza huduma za kusafirisha

mizigo kupitia meli hizi’ amesema Mhe. Silaa.

Mhe. Silaa ameitaka bodi hiyo kumlipa Mkandarasi Kampuni ya KTMI ambayo ndio

yenye   kandarasi   ya   kujenga   meli   hiyo   ili   kuepuka   madeni   ambayo   yanaweza

kuzalishwa kutokana na kucheleweshwa kwa  malipo.

Aidha, Mwenyekiti Mhe. Silaa ameipongeza  Bodi,  Menejimenti  na  Watumishi  wa

Kampuni   hiyo   kwa   kusimamia   vyema   miradi   inayotekelezwa   na   kuhakikisha

wahandisi wake wanapata ujuzi ili kuweza kusimamia vyema meli hizo mara baada ya

ujenzi na ukarabati kukamilika.


Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya MSCL, Meja Jenerali Mst. John Mbungo

amemuhakikishia   Mwenyekiti   wa   Kamati   ya   PIC,   Mhe   Silaa   kuwa   mradi   huo

utakamilika kwa wakati na tayari Kampuni imeshaweka mpango wa muda mfupi na

mrefu kwa wa namna fedha iliyowekezwa inaweza kurudi kwa kuhakikisha mzigo wa

uhakika unapatikana.

Naye Mtendaji Mkuu wa MSCL, Eric Hamis amesema mradi wa ukarabati wa MT.

Sangara   unatekelezwa   na   Kampuni   ya   KTMI   kutoka   nchini   Korea   Kusini   kwa

gharama   ya   takribani   shilingi   bilioni   8   na   kwa   sasa   umefikia   asilimia   90   na

unatarajiwa kukamilika mapema mwezi April mwaka huu.

Eric ameongeza kuwa miongoni mwa matokeo ya ukarabati huo mkubwa ni pamoja

kupungua kwa masaa ya safari ambapo utaiwezesha meli hiyo kusafirisha mzigo kwa

saa 6 tu ukilinganisha na hapo kabla ambapo ilikuwa inatumia saa zaidi ya 15 kwa

safari moja.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa MItaji iko Mkoani Kigoma ambapo

imepokea   taarifa   za   utendaji   wa   taasisi   za   WIzara   ya   Ujenzi   na   Uchukuzi   na

kutembelea miradi inayotekelezwa kwa mwaka 2022/23.

(Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi)

 


No comments