WENJE: NILITOROKA NCHINI NIKIWA NIMEVAA KAPTURA

Aliyewahi kuwa mbunge wa Jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza kupitia Chadema, Ezekiel Wenje, amesema alikimbia nchi baada ya uchaguzi mkuu mwaka 2020 akiwa amevaa kaptura.

Wenje alitoa kauli hiyo jana wakati wa mkutano wa hadhara wa kumpokea Godbless Lema, mbunge wa zamani wa Arusha mjini, aliyerejea toka uhamishoni nchini Canada.

Alisema alikimbia kuelekea Kenya na baadaye Canada, lakini yeye akawa wa kwanza kurejea ili kuja kusoma mazingira ambapo baada ya kujiridhisha akamshauri Lema naye arudi.

No comments