LEMA AMPA TANO RAIS SAMIA, ATAKA WANACHADEMA WASIMTUKANE

Mbunge wa zamani wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwa mwana demokrasia na kuwataka wafuasi wa Chadema kutomtukana kwani hawana sababu.

"Nimesikia kapita hapa kawapungia mkono, anajua nyinyi ni Chadema na mpo hapa mnamsubiri kiongozi wenu, hatutawafundisha kumtukana rais wala waziri mkuu, sisi tuwakosoe CCM kwa sababu lengo letu ni kuitoa madarakani," alisema.

Lema ambaye alirejea nchini baada ya kuishi kama mkimbizi huko Canada tangu baada ya uchaguzi wa 2020, alisema vitendo vya kufuatanafuatana ni undondocha na kusema kitendo cha Rais Samia kuwapungia mkono kimempa heshima mbele ya wanachadema.

No comments