MWAKILISHI JIMBO LA MTAMBWE AFARIKI
Mwakilishi wa Jimbo la Mtambwe Mkoa wa Kaskazini Pemba, Habib Mohamed Ali amefariki jijini Dar es Salaam.
Katibu wa Habari, Uenezi, Mawasiliano na Umma wa Chama cha ACT Wazalendo, ambacho ndicho alichokiwakilisha, Salim Bimani amesema taarifa zaidi itatolewa baada ya kuwasiliana na familia ya marehemu.
Alisema marehemu ambaye ni mmoja wa wanasiasa wakongwe nchini, alifariki wakati akiendelea na matibabu katika Hospitali ya SAIFEE jijini Dar es Salaam.

Post a Comment