WAZIRI AAGIZA RAIS WA ZAMANI WA YANGA AKAMATWE

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe ameagiza kukamatwa mara moja kwa aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Soka ya Yanga, Dkt Mshindo Msolwa baada ya mifuko 776 ya mchanga kukutwa katika kampuni anayoiongoza.

Katika msako wa Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoani Njombe, idadi hiyo ya mifuko ilikutwa katika ghala la kampuni ya usambazaji mbolea ya Minjingu ikiwa katikati ya mifuko ya mbolea.

Inahofiwa kuwa michanga hiyo huenda inatumika kuchakachua mbolea hivyo kupunguza ubora wake.

No comments