TEGETA BOXING ACADEMY KUWAPANDISHA MABONDIA WANNE ULINGONI MLIMANI CITY
Klabu ya ngumi ya Tegeta Academy, inayofundishwa na mkufunzi wake Ismail Kimito Mwita, itawapandisha mabondia wake wanne ulingoni katika mapambano yatakayopigwa kwenye Ukumbi wa Mlimani City Julai mwaka huu.
Mwita aliiambia Ojuku Blog kuwa klabu yake yenye mabondia 16, inajihusisha na kiinua vipaji vya vijana wa umri mbalimbali na nia yao ni kuwatengeneza ili wafikie viwango vya kuweza kushindana.
Aliwataja mabondia ambao watapanda ulingoni kuwa ni Yohana Daudi mwenye uzito wa kilo 72, Daud Israel (55kg), Zubery Ally (55kg) na Said Mohamed ambaye pia ana uzito wa kilo 55.
Klabu hiyo ipo chini ya Taasisi ya Mother Of Mercy Foundation inayomilikiwa na Gration Mbelwa (pichani) ambaye pia ni kada wa Chama Cha Mapinduzi.

Post a Comment