WALIMU WADUKUA MFUMO WA BENKI,WAIBA SHILINGI MILIONI 273 MWANZA

Walimu wanane wa shule za msingi na sekondari mkoani Mwanza wamekamatwa wakituhumiwa kudukua mfumo wa benki, kisha kujihamishia katika akaunti zao kiasi cha shilingi milioni 273.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa, amesema walimu hao walidukua Benki ya Walimu (MCB) na kuweza kujipatia kiasi hicho cha fedha, tukio ambalo walilifanya Februari 20 mwaka huu.

Alisema baada ya kuwafanyia upekuzi walimu hao walikutwa na fedha pamoja na mali zinazodhaniwa kuwa ni za wizi.

Wakati uchunguzi juu ya tukio hilo ukiendelea, kamanda aliwataja walimu hao na shule wanazotoka katika mabano kuwa ni Marwa Mwita ( Nyitundu primary), Gasper Maganga (Kilabela), Masaba Mnanka (Kilabela), Clever Banda (Nyamatongo Sec), Haroub Madia (Bugumbikiswa), Justin Ndege (Ishishangolo), Fredric Ndiege (Pamba C) na Steven Sambali wa shule ya msingi Nyangongwa.

No comments