VIGOGO WAWILI WA SERIKALI YA MAGUFULI MATATANI, WADAIWA KUTOROSHA FEDHA NJE
Vigogo wawili waliohudumu katika serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli, wapo matatani wakituhumiwa pamoja na mambo mengine kutoroshea mamilioni ya fedha nje ya nchi isivyo halali.
Vigogo hao, mmoja akiwa ni waziri wa wizara nyeti na mwingine akiitumikia ofisi kubwa iliyokuwa na uhusiano wa kikazi na Ikulu, wanadaiwa kutorosha fedha hizo ambazo zilipatikana kwa kuwalipisha watuhumiwa wa makosa kadhaa yakiwemo ya uhujumu uchumi, utakatishaji fedha na ukwepaji wa kodi.
Licha ya madai hayo ya kutorosha fedha, pia vigogo hao wanatuhumiwa kuwatisha watu waliotoa fedha hizo kwa namna mbalimbali, ikiwamo kuzuia wageni kufika majumbani mwao, wakihofia kutoa siri nje.
Vyanzo mbalimbali vya kuaminika, vinasema wawili hao walikamatwa na kuhojiwa na mamlaka na kwamba bado wapo chini ya mahojiano hadi sasa.

Post a Comment