WAKUTWA WAMEKUFA NDANI KWAO, WALIREJEA MIEZI MITATU KUTOKA MAREKANI WALIKOKUWA WAKIISHI

 

Polisi wa Nyamira nchini Kenya wanachunguza vifo vya watu wawili, mmoja mfanyabiashara aliyekuwa akiishi nchini Marekani na mkewe.

Wawili hao, Edward Morema Nyagechi, 62, na mkewe Mong’ina Morema, 60, walikutwa wamefariki ndani ya nyumba yao huko katika kijiji cha Getugi Jumanne asubuhi.

Bosi wa Polisi wa Masaba Kaskazini Robert Ndambiri alisema wapepelezi bado wanaendelea na uchunguzi ili kubaini waliohusika na mauaji hayo pamoja na sababu ya mauaji hayo.

Uchunguzi wa awali unaonyesha wawili hao waliuawa kwa kuwa marehemu walikutwa na wakiwa na majeraha kichwani na mwilini.

Polisi wanamshikilia msichana wa kazi pamoja na shamba boy.

Edward alirejea nyumbani kutoka Marekani miezi mitatu iliyopita na miili ya marehemu hao imepelekwa katika Hospitali ya Ichuni kwa uchunguzi zaidi.


No comments