VITA YA MESSI NA RODALDO SI YA KITOTO, ATABIRIWA KWENYE SAUDI ARABIA KWA TRILIONI 487
Mchezaji
Bora Duniani, Lionel Messi muda
wowote huenda akatua kwenye Klabu ya Al-Hilal inayoshiriki Ligi Kuu nchini
Saudi Arabia.
Hayo
yanajiri wakati baba mzazi ambaye pia ni wakala wa nyota huyo mzee, Jorge
Messi wiki iliyopita ameonekana Saudi Arabia jambo ambalo kama vile amekwenda
kuweka mambo sawa.
Kama
Messi, atakubali ofa ya pauni miloni 194 kwa mwaka kutoka kwa Al-Hilal hatua
hiyo inaweza kumfanya kuwa bilionea.
Mbali
na hilo Lionel Messi pia atamzidi mshindani wake Cristiano Ronaldo kuwa
mwanasoka anayelipwa pesa nyingi zaidi, wakati Mreno huyo akiwa analipwa pauni
milioni 175 kutoka Klabu ya Al-Hilal ya Saudi Arabia.


Post a Comment