WAKILI FATMA KARUME ATAMBA: KAMA SIKUMUOGOPA MAGUFULI, SEMBISE WAZUSHI?
Wakili machachari nchini, Fatma Karume ametamba kwamba kama hakuwahi kumuogopa Rais John Pombe Magufuli, basi hawezi kuwaogopa wazushi wanaomzushia.
Akiandika katika akaunti yake kwenye mtandao wa Twitter, wakili huyo ambaye baba na babu yake waliwahi kuwa marais wa Zanzibar, alisema wanaomzushia kuwa amejitokeza kuwatetea watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja hawana ukweli wowote.
Hata hivyo alisema endapo mashoga watamfuata na kutaka awatetee popote kisheria atafanya hivyo kwa kile alichokisema 'kumtetea anayebaguliwa siyo aibu'.
Hivi karibuni kumeibuka mjadala mkali katika eneo la Afrika Mashariki kuhusiana na ushoga, huku marais wa Uganda na Kenya kwa nyakati tofauti wakisema ndoa za jinsia moja hazitaruhusiwa katika nchi zao.

Post a Comment