URUSI YATISHIA KUZIHARIBU NDEGE ZA POLAND NA SLOKOVAKIA ZITAZOTOLEWA KWA UKRAINE

Wakati mataifa mawili ya Nato ya Poland na Slovakia yakiahidi kutoa ndege za kivita kuisaidia Ukraine inayopigwa na Urusi, taifa hilo kubwa la kisovieti limeaema litaziharibu ndege hizo mara zitakapoingia katika uwanja wa mapambano.

Poland imeahidi kutoa ndege nne aina ya Mig-29 za enzi ya Kisovieti, sawa na Slovakia iliyoahidi ndege 13 za aina hiyo.

Ndege hizo ndizo zinazoweza kurushwa na marubani wa Ukraine, kwani maombi yao ya ndege za kisasa aina ya Mid-16 kutoka Ulaya Magharibi yanashindikana kutokana na kuhitaji muda mrefu wa kujifunza kurusha.

Hivyo ndege hizo ambazo pia zilitengenezwa Urusi enzi za Sovieti, zinafahamika vyema na Russia na wataalam wanasema hazitatoa unafuu wowote kwa Ukraine kuhimili vishindo vya vita.


No comments