HUKO DUNIANI MAHAKAMA YA ICC YATOA HATI YA KUKAMATWA KWA PUTIN, MOSCOW YADHARAU

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu dhidi ya Binadamu maarufu kama ICC yenye makao makuu yake The Hegue, imetoa kibali cha kukamatwa kwa Rais wa Urusi, Vladimir Putin.

Mahakama hiyo imesema Putin, mpinzani mkuu wa nchi za Marekani na Ulaya Magharibi, anahusika na uhalifu wa kivita nchini Ukraine, ikiwa ni pamoja na kuwahamisha watoto wa taifa hilo kuwapeleka kwake.

Pamoja naye, mahakama hiyo pia imetoa hati za kukamatwa kwa maofisa kafhaa wa serikali yake.

Lakini Kremlin, ilipo Ikulu ya Putin, imesema hati hiyo haina maana yoyote.

Marekani na Ulaya wanaipinga Urusi kwa uvamizi wake Ukraine na zimeapa kwamba taifa hilo mwamba, halitashinda vita hivyo ambavyo vinaingia katika mwaka wake wa pili huku Ukraine, inayopigiwa upatu ijiunge na umoja wa kujihami wa Ulaya NATO ikiwa imeharibiwa vibaya.

No comments