MBWANA SAMATA, SIMON MSUVA KUUNGANA NA STARS MISRI

Nahodha Mbwana Samata na pacha wake katika safu ya ushambuliaji, Simon Msuva, wataungana na wachezaji wengine wa Taifa Stars nchini Misri tayari kwa pambano lao kuwania kufuzu kwa Afcon dhidi ya Uganda.

Taarifa zilizotolewa na TFF leo zinasema wachezaji 10 wa Stars walioitwa wanaocheza soka nje ya nchi, watatakiwa kujiunga na wenzao nchini humo badala ya kuja Dar es Salaam.

Uganda itacheza mechi hiyo huko katika Uwanja wa Suez Canal ikiwa kama mwenyeji, kwenye kundi ambalo linaongozwa na Algeria yenye pointi sita, ikifuatiwa na Niger huku timu hizo mbili za Afrika Mashariki zikishika nafasi ya tatu na nne.

Wengine watakaojiunga huko ni pamoja na Kelvin John, Novatus Disman na Himid Mao anayecheza hukohuko kwa mafarao.

No comments