URUSI WAMUAGA XI JINPING KWA AKUSHAMBULIA MIJI MITATU UKRAINE
Wakati Rais Xi Jinping wa China akiwa amemaliza mazungumzo na mwenzake Vladimir Putin, vikosi Vikosi vya Urusi vimeshambulia miji kadhaa ya Ukraine, na kuua
watu wasiopungua watatu katika shambulio la ndege isiyo na rubani kwenye eneo
la makazi la mkoa wa Kyiv.
Ghorofa za juu za
majengo mawili ya makazi zilishambuliwa mapema Jumatano katika jiji la
Rzhyshchiv, nje kidogo ya mji mkuu.
Mtoto wa miaka 11
alikuwa miongoni mwa waathiriwa kulingana na watoa huduma za uokoaji .
Kwengineko, maafisa
wa jimbo la Crimea linalodhibitiwa na Urusi walisema shambulio la ndege isiyo
na rubani ya Ukraine dhidi ya meli zao lilidhibitiwa.
Milipuko iliripotiwa
na wakazi katika mji wa bandari wa Sevastopol.
Mkuu wa mamlaka ya
uvamizi ya Urusi Mikhail Razvozhaev alisema "vitu" vitatu
vilivyolenga Meli ya Bahari Nyeusi vimeharibiwa na meli za kivita za Urusi
hazikuharibiwa.
Hakukuwa na maoni
yoyote kutoka kwa jeshi la Ukraine, ambalo lilisema mapema wiki hii lilikuwa
limeharibu makombora yaliyokuwa yanatumwa kwa meli hiyo katika kituo cha reli
huko Dzhankoi kaskazini mwa Crimea.
Rais wa Ukraine
Volodymyr Zelensky alisema Urusi imerusha zaidi ya ndege 20 zisizo na rubani,
pamoja na makombora.
Akizungumzia
kuondoka kwa Rais wa China Xi Jinping kutoka Urusi saa kadhaa kabla, alisema
kwamba kila wakati "mtu anapojaribu kusikia neno 'amani' huko
Moscow," amri nyingine ilitolewa kuanzisha mashambulizi.


Post a Comment