UGONJWA ULIOIBUKA KAGERA WATAMBULIKA
Serikali ya Tanzania imethibitisha kupatikana kwa virusi vya
homa ya Marburg katika mkoa wa Kagera uliopo Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo.
Mnamo tarehe 16
March 2023, wizara ya afya ilitoa taarifa kwa umma juu ya ugonjwa ambao
haukufahamika mara moja ambao uliambukizwa kwa watu mbalimbali.
Hata hivyo Tanzania
imesema imefanikiwa kuuzuia ugonjwa huo kutoka nje ya mipaka ya mkoa wa Kagera.
Ugonjwa wa ajabu
uliosababisha vifo vya watu watano kati ya wanane waliougua wilayani Bukoba
Vijijini mkoani Kagera umetambuliwa kuwa ni Marburg.
Taarifa imesema ugonjwa huo huambukizwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine au kutoka kwa mnyama kwenda kwa binadamu.



Post a Comment