URUSI, CHINA NA IRAN ZAANZA MAZOEZI YA PAMOJA YA KIJESHI
Katika hali inayozidi kutishia amani ya dunia Urusi imeanza mazoezi ya kijeshi ya baharini na washirika wake wa karibu,China na Iran.
Mazoezi hayo ambayo ni tishio kwa Marekani na washirika wake wa NATO yatafanyika katika Bahari ya Arabia na yamepewa jina la Marine Security Belt 2023.
Mazoezi hayo yatahusisha meli za kivita za kivita za Urusi aina ya Admiral Goshkov na yatahusisha kurushwa kwa mizinga mchana na usiku.
Wachambuzi wa masuala ya kijeshi wanaona zoezi hilo la kijeshi, wakati huu mzozo wa Urusi na Ukraine ukiendelea, ni tishio jipya kwa usalama wa dunia.
China na Iran zimekataa kupiga kura azimio la kuishutumu Urusi kwa uvamizi wake nchini Ukraine wakati vita vikiingia mwaka wa pili sasa.

Post a Comment