TETESI: HAJI MANARA ASAMEHEWA NA TFF, FEI TOTO AREJEA YANGA
Mitandao ya kijamii kila siku linaibuka jambo jipya linalowahusu mastaa wa fani mbalimbali.
Leo, mitandao imesheheni kuwa kiungo fundi wa Yanga aliyesusa, Zanzibar Finest, Fei Toto amerejea klabuni hapo baada ya kukaa mezani na viongozi wake na kulimaliza suala lake kiutu uzima.
Zanzibar Finest alisusa miezi takriban mitatu iliyopita, akilalamikia ujira mdogo tofauti na kazi kubwa anayohisi kuifanya kwa mabingwa hao wa kihistoria katika soka nchini.
Kana kwamba haitoshi, stori mitandaoni bado zipo jangwani zikidai kuwa Bughat, Haji Manara amesamehewa na Shirikisho la Soka nchini, ambalo lilimfungia kwa muda ili asijihusishe na mambo ya soka, kwa3 kosa la kupitiliza kwa majukumu yake wakati huo akiwa msemaji wa Yanga.

Post a Comment