KAMISHNA MADAWA YA KULEVYA ONDOLEWA, AWA RAS RUKWA
Kamishna Gerald Kusaya, aliyekuwa Kamishna wa Mamlaka ya Udhibiti wa Madawa ya kulevya, ameondolewa katika nafasi hiyo na kumpeleka kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa na nafasi yake imejazwa na Aretas James Lyimo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu leo, Rais Samia Suluhu Hassan pia amewateua makatibu tawala wa mikoa mitatu, Ally Senga Gugu anakuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma. Gugu alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara.
Tixon Tuyangire Nzunda ameteuliwa kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Kilimanjaro, akichukua nafasi ya Willy Machumu aliyestaafu.


Post a Comment