UMOJA WA WANAWAKE WA CCM WAMPONGEZA RAIS SAMIA MIAKA MIWILI YA UONGOZI WAKE
Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) leo umeandaa sherehe maalum ya kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutimiza miaka miwili tangu alipopewa dhamana ya kuliongoza taifa, kufuatia kifo cha mtangulizi wake, Hayati John Pombe Joseph Magufuli.
Katika sherehe hizo zinazofanyika katika Uwanja wa Uhuru uliopo Temeke jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa UWT Taifa, Mary Chatanda ametoa hotuba ya kumpongeza.
Amemsifu kwa kuweza kuhudhuria kongamano lililoandaliwa na Baraza la Wanawake wa Chadema ( Bawacha) mapema mwezi huu na kusema kitendo hicho kilionyesha namna ambavyo siasa siyo uadui.
Aidha Mary Chatanda ametaka kuwepo na sheria ambayo itawabana watu wanaohusika na ukatili wa kijinsia na ushoga ili wahasiwe.
Leo Mama anatimiza miaka miwili tangu alipoapishwa Machi 19 mwaka 2021 kushika wadhifa huo, mkubwa kuliko yote nchini Tanzania.

Post a Comment