DONALD TRUMP KUKAMATWA KWA KESI YA KUMHONGA KAHABA ALIYETEMBEA NAYE

Rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump atakamatwa Jumanne ijayo ili aweze kushtakiwa kwa tuhuma za kumhonga mcheza filamu za ngono aliyetembea naye ili asifichue uhusiano wao.

Trump ambaye anataka kujaribu kurejea White House kwa mara ya pili katika uchaguzi wa mwakani akiiwakilisha Republican, ameandika katika akaunti yake ya mtandao wa Social kwamba waendesha mashtaka wa New York wanakusudia kufanya hivyo.

Waendesha mashtaka hao kwa zaidi ya miaka mitano wamekuwa wakifanya uchunguzi juu ya madai ya mcheza filamu huyo kuwa aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Trump kabla yajaingia Ikulu.

Aliibua madai hayo wakati wa harakati za uchaguzi wa 2016, na alidai wakili wa Trump, Michael Cohen ndiye alimkabidhi kitita cha dola 130,000 ili kumfumba mdomo. Trump alishinda uchaguzi huo.

Stomy Daniels, alisema alipewa hela hizo ili kuficha uhusiano kati ya wawili hao. Endapo atakamatwa, itakuwa ni mara ya kwanza kwa aliyewahi kuwa rais wa Marekani kushtakiwa kwa makosa ya jinai na itakua na athari kubwa kwake katika kuwania kiti hicho kwa mara ya pili.

No comments