STAMFORD BRIDGE KUVUNJWA, KUJENGWA UPYA
Mmiliki wa timu ya Chelsea, Todd Boehly anafikiria kufanya uwekezaji mpya kwa kuuvunja na kuujenga upya uwanja wa Stamford Bridge ambao ni nyumbani kwa klabu hiyo tangu mwaka 1905.
Kiasi cha paundi bilioni mbili za Uingereza zinatarajiwa kutumika, ambazo ni zaidi ya shilingi trilioni tano za kitanzania katika mradi huo unaotarajiwa kukamilika msimu wa 2030.
Kwa muda wote wa miaka minne ya ujenzi huo, kikosi hicho kitachagua kutumia moja kati ya viwanja vitatu vya Clavven Cottage, Twiekenhan au Wembley kama uwanja wake wa nyumbani.

Post a Comment